Friday, 7 November 2014

DANGOTE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KIWANDA CHAKE KIKUBWA CHA SARUJI MJINI MTWARA

Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akiteremka toka kwenye ndege alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara, kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha saruji kinachojengwa mkoani humo.

Dangote akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Baruti (kushoto)

Dangote akisalimiana na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa

Dangote akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa kampuni ya Dangote nchini, Esther Baruti na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa.

Dangote akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma, baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa kiwanda.

Alhaji Aliko Dangote akitabasamu baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa kiwanda hicho.
Dangote akitumia gari kukagua ujenzi wa kiwanda hichoMwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote akiwa kwenye gari huku akipata maelezo ya ujenzi wa kiwanda hicho kutoka kwa mafundi na wahandisi ya Dil & Sinoma inayojenga kiwanda hicho kitakachokuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.

Msafara wa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote, ukikagua ujenzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwakuanza kazi Aprili, mwakani. Awamu ya kwanza ya kiwanda hicho ujenzi wake ukikamilika kitakuwa kinazalisha tani 6000 kwa siku.

Dongote akiagana na Kaimu Mkuu wa Mkoawa Mtwara, Ponsiano Nyami

Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote, akiaga alipokuwa akiondoka na ndege yake kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara jana. Alitumia takribani saa mbili kuwepo nchini, baada ya kuwasili asubuhi saa 1:42 na kuondoka saa 3:42 baada ya kupata maelezo ya ujenzi na kukagua kiwanda chake.

Thursday, 6 November 2014

MH. RAIS KIKWETE WAAPISHA MAKATIBU WAKUU, MABALOZI, WAKUU WA MIKOA PAMOJA NA MAKATIBU TAWALA WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mh. Samwel William Shellukindo kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais katika Masuala ya Diplomasia leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mh. John Vianney Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Mkuu waRais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mh. Halima Omary Denengo kuwa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Dkt Ibrahim Hamisi Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi leo Ikulu jijini Dar es salaam.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpatia vitendea kazi Dkt Yohana Budeba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Injinia Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Dkt Donan Mmbando kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Charles Pallangyo kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Geita Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Bw, Adoh Stephen Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wapya baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Balozi mpya wa Tanzania Nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka (wa pili kushoto), pamoja na mabalozi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao ni kutoka kushoto Balozi Joseph Sokoine (Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika). Balozi Yahaya Simba (Mkurugenzi idara ya Mashariki ya Kati na Balozi Celestine Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa.

HAKATI ZA KUMPATA KIONGOZI WA KIRAIA WA MPITO ZAANZA NCHINI BURKINA FASO

Mkutano wa wadau katika mchakato wa kutafuta serikali ya mpito ya Burkina Faso

Wanadiplomasia wanaowawekea shinikizo viongozi wa jeshi la Burkina Faso kukabidhi madaraka kwa raia, wameanza mchakato wa kumtafuta mtu atakayeongoza serikali ya mpito hadi uchaguzi utakapofanyika.
MMazungumzo hayo ya jana yalisimamiwa na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria, John Dramani Mahama wa Ghana na Macky Sall wa Senegal, yakiwashirikisha maafisa wa jeshi, viongozi wa vyama vya kisiasa na wawakilishi wa asasi za kiraia.

Ingawa washiriki waliafikiana juu ya kuwepo kwa utawala wa mpito kwa kipindi cha mwaka mmoja, ambao utaongozwa na raia, hakukuwapo makubaliano juu ya kiongozi wa kipindi hicho. Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliwaachia jukumu hilo wahusika nchini Burkina Faso.
''Na mtaendelea hadi pale mtakapompata mtu kutoka nchi hii, mwenye haiba, heshima, uaminifu na uzalendo ambaye ataweza kuiongoza Burkina Faso hadi mwakani, kwenye uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika. Hilo ndilo jukumu tunalowaachia kutekeleza.'' Alisema rais Mahama.

Rai ya kuepuka vikwazo


Rais wa Ghana John Dramani Mahama akitoa rai katika mkutano huo

Rais Mahama alisema anaamini mchakato wa kumpata kiongozi huyo hautachukuwa wiki kadhaa, na kueleza matumaini yake kwamba haitakuwa lazima kwa jumuiya ya kimataifa kuiwekea vikwazo Burkina Faso. Umoja wa Afrika uliwapa wanajeshi wa Burkina Faso muda wa wiki mbili kukabidhi madaraka kwa raia, la sivyo wakabiliwe na vikwazo vya kiuchumi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon aliunga mkono juhudi za marais hao kutafuta suluhisho la amani katika mzozo huo wa Burkina Faso. Msemaji wake Stephen Dujarric amesema Umoja wa Mataifa unashirikiana na Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, kutafuta suluhisho la kudumu linalowahusisha wadau wote nchini humo.

Hali kadhalika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema pia linaunga mkono mchakato huo, na kuwataka wanajeshi kukabidhi madaraka na kuheshimu katiba ya nchi bila kuchelewa.

Ishara ya mvutano


Luteni Kanali Isaac Zida anayeshinikizwa kukabidhi madaraka kwa viongozi wa kiraia

Hata hivyo katika kile kilichochukuliwa kama ishara ya kupanda kwa joto la mvutano katika mkutano huo, wanasiasa wa upinzani pamoja na wanaharakati walitoka nje baada ya maafisa wa chama kilichokuwa madarakani kuingia katika mkutano huo.
Kiongozi wa asasi za kiraia Mathias Tankoano alisema hawawezi kukaa chumba kimoja na watu wanaotuhumiwa kusababisha vifo vya watu ambao hata bado hawajazikwa, na kuongeza kuwa maafisa hao wanapaswa kuhukumiwa kwa vifo hivyo, na kwa hila zao dhidi ya katiba ya nchi ambazo zililipeleka taifa katika ghasia.

Taarifa zilizotolewa baadaye zilisema Assimi Kouanda, kiongozi wa chama cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore alikamatwa na polisi baada ya kutoa matamshi ambayo yanaweza kuvuruga utulivu wa umma.
Burkina Faso iliingia katika mzozo wiki iliyopita baada ya kuibuka kwa maandamano yenye ghasia, kufuatia hatua ya aliyekuwa rais wake Blaise Compaore kujaribu kubadilisha katiba ili aweze kugombea mhula mwingine, kuendeleza utawala wake wa miaka 27. Baada ya kiongozi huyo kuikimbia nchi, aliyekuwa naibu kamanda wa kikosi cha kumlinda, Luteni Kanali Isaac Zida aliteuliwa na jeshi kuchukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo.

MH. KINANA AKUTANA NA BALOZI WA RWANDA NCHINI TANZANIA,


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha Balozi wa Rwanda hapa nchini bwana Eugene Kayihura, kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Balozi huyo Ernest Bugingo.


Balozi wa Rwanda hapa nchini Eugene Kayihura, akijitambulisha kwa Katibu Mkuu wa CCM Mh. Abdulrahman Kinana, kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Balozi huyo Ernest Bugingo.


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Balozi huyo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) akimsindikiza mgeni wake Balozi wa Rwanda hapa nchini Eugene Kayihura, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Balozi huyo Ernest Bugingo.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akiagana na Balozi wa Rwanda hapa nchini Eugene Kayihura, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Wednesday, 5 November 2014

SEMINA YA SDG'S IKIENDELEA



Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.

SEMINA YA SDG'S IKIENDELEA



Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.

SEMINA YA SDG'S YAFANYIKA ZANZIBAR



Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee akifungua rasmi warsha ya siku moja ya iliyohusisha wadau mbalimbali wa maendeleo, kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs), iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) iliyofanyika hivi karibuni visiwani Zanzibar. Kulia kwake ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Zanzibar katika kuangalia masuala muhimu yanayohusu muktadha ujao wa kufanikisha uondoaji wa umaskini uliotopea (SDGs) baada ya kukamilika kwa programu ya maendeleo ya milenia (MDGS).
Alisema kitendo cha serikali kuandaa warsha ya kupashana kuhusu programu hiyo mpya kabla ya mazungumzo na mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo ni washirika wa maendeleo kuhusu SDGs kunaonesha dhamira ya dhati kwa serikali kuendelea kusukuma mbele maendeleo yenye lengo la kunemeesha wananchi.
Mratibu huyo alisema hayo hivi karibuni katika warsha iliyofungulia na Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee iliyokusanya wadau mbalimbali wa maendeleo kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs),iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF).
Warsha hiyo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Programu wa ESRF Dk. Tausi Kida warsha hiyo ni sehemu ya kuelezana kuhusu mkakati huo mpya wa Umoja wa Mataifa unachukua nafasi ya MDGs na nafasi ya Tanzania katika kutekeleza malengo hayo ya kimataifa.

MH. RAIS PIA ATEUA MAKATIBU WAKUU



Kadhalika, Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua wanne wapya na kuhamisha mmoja, uteuzi uliomuondoa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo.
Pallangyo sasa anakua Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, nafasi ambayo inatafsriwa kuwa adhabu, siku chache baada ya vyombo vya habari ikiwamo FikraPevu kuibua kashfa ya uhaba wa dawa katika hospitali kubwa za serikali.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.

Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa walioteuliwa ni pamoja na Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuchukua nafasi ya Pallangyo.

Katika uteuzi huo Dkt. Yohana Budeba anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba amepanda na kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro anahamishiwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA kuchukua nafasi ya Dkt. Meru.
Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.

MH. RAIS AFANYA UTEUZI NA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA

Friday, 3 October 2014

KINANA ZIARANI MJINI TANGA


Abduruhaman Kinana akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM mjini Tanga wakati was ziara take mjini hump.

Mh. Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa chama mjini Tanga mjini humo

Kina mama wenye nyuso za furaha wakimshangilia Mh. Kinana.