Wednesday, 5 November 2014

SEMINA YA SDG'S YAFANYIKA ZANZIBAR



Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee akifungua rasmi warsha ya siku moja ya iliyohusisha wadau mbalimbali wa maendeleo, kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs), iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) iliyofanyika hivi karibuni visiwani Zanzibar. Kulia kwake ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Zanzibar katika kuangalia masuala muhimu yanayohusu muktadha ujao wa kufanikisha uondoaji wa umaskini uliotopea (SDGs) baada ya kukamilika kwa programu ya maendeleo ya milenia (MDGS).
Alisema kitendo cha serikali kuandaa warsha ya kupashana kuhusu programu hiyo mpya kabla ya mazungumzo na mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo ni washirika wa maendeleo kuhusu SDGs kunaonesha dhamira ya dhati kwa serikali kuendelea kusukuma mbele maendeleo yenye lengo la kunemeesha wananchi.
Mratibu huyo alisema hayo hivi karibuni katika warsha iliyofungulia na Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee iliyokusanya wadau mbalimbali wa maendeleo kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs),iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF).
Warsha hiyo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Programu wa ESRF Dk. Tausi Kida warsha hiyo ni sehemu ya kuelezana kuhusu mkakati huo mpya wa Umoja wa Mataifa unachukua nafasi ya MDGs na nafasi ya Tanzania katika kutekeleza malengo hayo ya kimataifa.

No comments: