Tuesday, 3 March 2015

VIONGOZI WA CCM TAIFA WAWASILI MJINI SONGEA TAYARI KWA MAZISHI YA MAREHEMU CAPTAIN KOMBA


Katibu mkuu wa CCM Taifa Mh. Abdulhaman Kinana akiwasili Mjini Songea leo kwa ajili mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Mgharibi Mh. John Komba




Naibu katibu mkuu wa CCM Taifa na naibu waziri wa Fedha wa Tanzania Mh. Mwigulu Nchemba wakisalimiana na wakazi wa mjini Songea alipowasili kwa ajili ya mazishi ya marehemu John Komba. 

Mwanamuziki mashuhuru wa Taarabu Bi. Khadija Kopa akiwasili mjini Songea leo



MKUU WA MKOA WA RUVUMA AKIWAONGOZA WANANCHI WA SONGEA KUAGA MWILI WA MAREHEM JOHN KOMBA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma akiongoza maelfu ya wakazi wa Songea kutoa salam za rambi rambi za mkoa

MWILI WA MH. CAPTAIN JOHN KOMBA WAWASILI MJINI SONGEA


Mwili wa marehemu John Komba ambae alikuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM ukiwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Songea leo.

KATIBU MWENEZI WA CCM TAIFA MH. NAPE MNAUYE AKISHIRIKI KATIKA WIMBO WA KUMUAGA MAREHEMU CAPTAIN KOMBA




Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Mh. Nape Nnauye, Mbunge wa Viti Maalum na mkoa wa Singida Martha Mlata wakishirikiana na mwanamuziki mkongwe King Kikii, Lwiza Mbutu na wasanii wengine kuimba wimbo maalum wa kumuenzi marehemu Kapteni John Komba wakati wa kutoa heshima za mwisho kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Tarehe 2 Machi 2015.

NAPE AONGOZA WANAMUZIKI WA DANSI KUIMBA WIMBO MAALUM WA KUMUENZI KAPTENI...