Tuesday, 18 October 2011

HIVI NDIVYO CCM INAVYOPENDWA NA KUHESHIMIWA.

Hawa ni baadhi tu ya watu miongoni mwa wengi wenye imani kubwa na chama tawala.

KIWETE AWASILI RUVUMA KUFUNGUA KONGAMANO.

Rais JK Kikwete akiwa amembeba moja ya watoto waliofika uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Ruvuma kumraki. Mh rais yuko mpanda kwa ajili ya ufunguzi wa kongamano la uwekezaji kwenye ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Friday, 14 October 2011

WAKENYA; MW. NYERERE NI KAMA MALAIKA WETU.

TUNAPOFANYA kumbukumbu ya miaka 12 tangu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere atutoke, hapana shaka wengi wanamkumbuka kwa yale aliyoyafanya kwa nchi yake.
Yumkini, wengine wanatafakari ya kuwa labda,angekuwepo - pengine hekima zake zingeweza kuliokoa taifa hili ambalo linaonekana kutumbukia zaidi katika umaskini.
Wanaharakati wengi wa wakati ule, wanamzungumzia Baba wa Taifa kwa namna mbalimbali.
Mmoja wao, Mwandawiro Mghanga, mbunge wa zamani wa jimbo la Wundanyi nchini Kenya na mwanafalsafa wa Ujamaa ana mengi ya kusema kuhusu Nyerere.
Mghanga anasema, kwa juhudi alizozifanya Mwalimu, alistahiki tuzo ya heshima (Nobel Prize), lakini mpaka mauti yanamfika, hakuwahi kupata tuzo hiyo. Na badala yake, wanapewa viongozi wengine ambao hata hawajafanya kazi nzito kama ya kiongozi huyo.
“Nyerere alitetea haki za wana Afrika. Hakutetea hata siku moja siasa za ubeberu, na kwa sababu hao mabeberu ndiyo hutoa tuzo hizo, kwa makusudi walimnyima,” anasema Mghanga na kuongeza: “hakupewa tuzo ya heshima kwa sababu aliupinga ubepari.”
Mghanga, anauzungumzia mustakabali wa Tanzania tangu Mwalimu Nyerere atutoke na anasema, Tanzania inaonekana kama imeelemewa mzigo wa matatizo ambayo haiwezi kuyatatua. Na hiyo ni kwa sababu imetetea siasa za ubepari.
Anazitaja siasa za ubepari kuwa ni siasa za matumbo na ndiyo maana, viongozi wachache wanafaidi huku wananchi wakiteseka.
“Tangu waingie hawa viongozi baada ya Nyerere(anawataja Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na sasa Jakaya Kikwete) wameileta sera ya ubinafsishaji. Na matokeo yake, viwanda, mashirika ya umma vyote vimebinafsishwa,”Anasema.
Mghanga, ambaye mpaka saa bado yungali katika harakati za kulijenga bara la Afrika anasema, hata yeye mwenyewe amekula matunda ya nguvu za Nyerere. Watoto wake anasema walipata elimu bure katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hali kadhalika yeye.
Anaongeza: “Nilipofukuzwa na Jomo Kenyata hapa Kenya, nilikwenda kuishi kule (Tanzania) na niliishi kwa amani. Tulikuwa tukipewa ruzuku ya vyakula kila mara,”
Anasema wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa kama ilivyo sasa. Hivi sasa anaziona chembechembe za ukabila na udini.
“Kama kuna vitu ambavyo Tanzania inabidi ivishike kwelikweli, basi ni vita vya ukabila na udini. Hivyo ndivyo baba wa taifa alivyofanikiwa kuviondoa katika taifa hilo,” Anasema.

Mghanga ambaye anadai alikuwa rafiki wa karibu wa Nyerere anasema, wakati wake (Nyerere) hakukuwa na chembe ya ufisadi. Anasema anashangazwa na jinsi viongozi wa sasa wanavyojilimbikizia mali wakati Baba wa Taifa hakufanya hivyo hata kidogo.
Pia, anazungumzia Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977 wakati ule ikiwa chini ya Milton Obote wa Uganda, Jomo Kenyata wa Kenya na Nyerere kwa Tanzania.
“Kenyata ndiye aliyechangia kuvunjika kwa jumuia ile kwa kuwa alipendelea siasa za kibepari. Obote na Mwalimu walisimamia katika ujamaa. Basi, mpishano ule ndiyo uliangusha EAC,” anasema Mghanga
Anaitaja jumuia ya sasa na kusema, inakwamishwa na Watanzania ambao bado wanaweka vikwazo kadhaa vya kiuchumi na kisiasa.
Naye Waziri wa Huduma za Matibabu Kenya, Profesa Anyang’ Nyong’o anamtaja Nyerere kuwa alikuwa ni binadamu lakini ni mfano wa malaika.
Anasema, wakati huu taifa linapokumbuka kifo cha Mwalimu, basi wakumbuke kitu kimoja cha muhimu kuliko vyote alichokifanya … nacho ni ‘ukabila’
“Kama kuna kitu cha muhimu alichokifanya Mwalimu, basi ni kutembea Tanzania nzima akihimiza Watanzania wawe kitu kimoja na kuutokomeza ukabila.
Kwa hilo Watanzania hamna budi kumuombea kila siku,” anasema Prof. Nyong’o.
Waziri huyo anasema, nchi nyingine za Afrika Mashariki, zinaionea wivu Tanzania kwa kuwa hakuna ukabila, hivyo anawasihi watanzania, pamoja na mengine, wadumishe hilo zaidi.
Anatolea mfano mapigano ya kisiasa yaliyotokea nchini Kenya mwaka 2007 na kusema, yalikuwa ni ya kisiasa lakini yalichochewa zaidi na ukabila.
Nyong,o amfananisha Nyerere na malaika
Anasema, akiwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, anakumbuka kusikia hotuba ya Nyerere iliyokuwa ikitaka Afrika Mashariki iwe taifa moja.
“Alikuwa tayari kuiacha Tanganyika ichelewe kupata uhuru wake , ili Kenya na Uganda nazo zipate na baadaye nchi za Afrika Mashariki ziwe taifa moja. Alijitoa mhanga kweli kweli,” anasema Prof Nyong’o
Anasema, kilichokwamisha hayo ni wimbi zito la ubwanyeye lililokuwepo nchini Kenya na mzimu huo ndiyo ulioitafuna hata Jumuiya ya Afrika Mashariki baadaye.
Prof Nyong’o anahitimisha mazungumzo yake na kusema, roho ya Nyerere inalitazama taifa la Tanzania linapokwenda na hapana shaka kuwa, inalia kwa huzuni kwani yale aliyoyahimiza kiongozi huyo yanaonekana kwenda mrama.
Anaeleza kuwa Nyerere alipenda kusisitiza, kuhusu kupigana na maadui watatu: ujinga, umaskini na maradhi. Mambo ambayo kwa kiasi kikubwa bado yamevijaza vyumba na korido za taifa hili.
Mawazo ya mwanahabari, mhariri wa zamani na mwanachama wa toleo la Kenya (Kenya Year Book), Philip Ochieng, hayakutofautina kwa kina na Wakenya wengine wa wakati ule. Ochieng naye anamsifu Nyerere kwa kuutokomeza ukabila.
Anasema, Mwalimu Nyerere aliua kabisa ukabila, jambo ambalo Kenya imeshindwa na tayari limekwishaigharimu nchi hiyo.
“Nimefanya kazi Tanzania katika gazeti la serikali wakati huo, nikiwa pamoja na rais wa zamani, Benjamin William Mkapa. Sikuwahi kusikia Watanzania wakizungumzia ukabila hata mara moja,” anasema Ochieng.
Anasema jambo la msingi ambalo Mwalimu alishindwa ni siasa za Ujamaa. Anasema, endapo Nyerere angetazama mbele na kuona kuwa kuna kitu kinaitwa ‘utandawazi’ kinakuja, basi angetambua kuwa ujamaa ni kazi ngumu.
Anasema utandawazi na ujamaa ni kama mafuta na maji na kamwe haviingiliani.
“Waliokuwa wakitetea ujamaa wakati ule ni wachache, Kingunge Ngombale Mwiru, Rashid Kawawa na Nyerere, hivyo wazo hilo lilikosa hamasa na uongozi makini. Hilo ndilo lililofanya Tanzania ikawa nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na Kenya au hata Uganda,” anasema Ochieng.
“Tanzania ilikuwa ni nchi yenye makabila zaidi ya 100 ambayo yalipoteza uhuru wake, lakini taifa moja likauleta uhuru huo,” (Mwalimu J.K Nyerere, Chuo Kikuu chaToronto, Canada, 1969)
Hakika, hatuna budi kudumisha umoja na mshikamano kama alivyotuasa baba wa Taifa na katu tusiruhusu ukabila na udini ukaingia Tanzania.
 

MAADHIMISHO YA UWT KUSHEREHEKEA UHURU YAFANA.

Mama Salma Kikwete na bi. Fatuma Karume akiangalia bidhaa mbalimbali zilizoletwa na kinamama kutoka maeneo kadhaa nchini
Mama Fatma karume ambaye ni mmoja ya waasisi wa UWT akifurahia zawadi ya tuzo aliyopewa
na waandaaji wa sherehe hizo.
Mama Kikwete akiwasalim mamia ya akina mama waliofika katika maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi mama Salma Kikwete akiwasili mkutanoni hapa wakati maadhimisho hayo.
Katibu mkuu wa UWT bi. Amina Makillagi aliyeshika mic akimtambulisha moja ya waasisi wa jumuiya huyo Dr. Msimu Abdurhaman Hassan aliyekuwa mmoja ya wageni waalikwa.
Baadhi ya kinamama wakipita mbele ya mgeni rasmi na mabango yenye ujumbe mbalimbali kina inavyoonekana kwenye picha hii.

MH. PINDA MKUTANONI NCHINI MAREKANI.

Rais wa zamani wa Brazil bw. Luiz Lula akiwa na waziri mkuu Pinda wakionyesha kitabu baada ya rais huyo kumzawadia mh. pinda jana huko Iowa.
Waziri mkuu mh. Pinda akiwa na rais wa World Food Prize bw. Kenneth Quinn wakifurahi jambo wakati wa mapumziko. Pinda yuko nchini Marekani ambapo anahudhuria mkutano huo wa World Food Prize.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. Benard Membe wakiwatambulisha mabalozi na maafisa mbalimbali kwa mama Maria Nyerere waliofika nyumbani kwa hayati baba wa taifa Mw. Nyerere Butiama.

Thursday, 13 October 2011

Mama Maria Nyerere akipokea zawadi toka kwa balozi wa India nchini Tanzania bw. Bhagiralt K.V, nyuma ya balozi huyo wa India ni baadhi ya mabalozi na wageni kadhaa walifika nyumbani kwa baba wa taifa hayati Mw. Julius K. Nyerere Butiama kwa ajili ya kusalim mama Maria Nyerere.

WAZIRI MKUU MSTAAFU AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA TBL.

Waziri mkuu mstaafu Mh. Cleopa D, Msuya akihutubia katika mkutano wa mwaka wa kampuni ya uzalishaji na uuzaji  bia maarufu kama TBL jana jijini Dar es saalam, kushoto ni katibu muhktasi wa kampuni hiyo bw. Haluna Ntahena na kulia ni mkurugenzi mtendaji wa TBL bw. Robin Goetzsche.

Wednesday, 12 October 2011

Dr. SHAIN AKABIDHI ZAWADI KWA WALIOFANYA VYEMA KATIKA MITIHANI YA SECONDARI

Mh. Shain ambaye ni rais wa Zanzibar akikabizawadi kwa wanafinzi wa kidato cha nne na cha sita waliofanya vizuri kwa mwaka wa masomo wa 2010 - 2011

WAKIMBIZI WA KI-ZANZIBARI WALIOKO SOMALIA WAILALAMIKIA TANZANIA KWA KUTOWARUDISHA NYUMBANI.

Mogadishu kuna mapigano Wakimbizi kutoka visiwa vya Zanzibar wamekwama katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wakidai serikali ya Tanzania imeshindwa kutoa kibali kwa shirika la wakimbizi duniani UNHCR ili kuwarejesha makwao.

Wakimbizi hao walikimbilia Somalia miaka kumi iliyopita baada ya machafuko ya baada ya uchaguzi wa urais wa Zanzibar mwaka wa 2000 Wakimbizi hao kutoka visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania wameiambia BBC kuwa mwezi Januari mwaka huu, shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR lilianzisha uratatibu wa kuwasajili kwa lengo la kuwarejesha makwao kwa hiari.

Wakati huo shirika la UNHCR liliwafahamisha wakimbizi hao wapatao 100 kuwa watarejeshwa nyumbani baada ya miezi mitatu, lakini hadi sasa mpango huo haujatimia. "Baada ya muda huo wa miezi mitatu kumalizika, UNHCR ilituambia kuwa serikali yetu ya Tanzania haijatoa kibali cha kutuwezesha kurejea nyumbani na haitowezekana kuendelea na safari bila ya kupata kibali hicho.

Amesema mmoja wa wakimbizi hao Mohamed Adam Suleiman. Bw Suleiman ametoa wito kwa serikali ya Tanzania kutoa kibali cha safari kwa UNHCR ili waweze kurejea nyumbani. "Tunatoa wito kwa serikali ya Tanzania kutufahamisha sisi na Watanzania wengine sababu ya kushindwa kutoa kibali hicho. Pengine wana sababu zao za msingi, lakini sisi ni wakimbizi ambao tuna haki ya kurejea nyumbani."

Wakimbizi hao walikimbia machafuko ya baada ya uchaguzi visiwani Zanzibar mwaka wa 2000, baada ya kuzuka kwa mzozo juu ya matokeo ya uchaguzi wa urais, ambapo mgombea wa CCM aliibuka mshindi. Wengi wa wakimbizi hao walikuwa wafuasi wa chama cha upinzani cha CUF, na walipitia Kenya na kuishi kwa muda mfupi, kabla ya kuelekea Somalia mwezi Septemba mwaka 2001.

Kufuatia muafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar mwaka uliopita, na uchaguzi ambao ulimpa nafasi kiongozi wa CUF, Seif Shariff Hamad kuwa makamu wa rais, wakimbizi hawa wameamua kukubali kurejeshwa makwao. Awali idadi ya wakimbizi hawa waliokwenda Mogadishu ilikuwa mia mbili, lakini baadhi yao wamerejea nyumbani na wengine kwenda katika mikoa mingine nchini Somalia kufanya kazi mbali mbali.

DICOTA CONVETION WASHINGTON DC

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Benard Membe akiwa katika picha ya pamoja na waandaji na baadhi ya washiriki wa mkutano wa DICOTA uliofanyika hapa United State
Sept 22-25/ 11. Kutoka kushoto ni bw. Richard Kusesela, Dr. Reonard Tenende, Dr Switbert Mkama,
Mh. Benard Membe, Hilary Rite, Dr. Crispin Semakule na bw. Erick Mahai.

TOFAUTI NA MAKUNDI NDANI YA CCM ZA MKERA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM - TAIFA.

Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mh. Nape Mnauye akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine alielezea kukerwa kwame na makundi ndani ya chama tawala CCM. Kwa taarifa zaidi tafadhari tembelea website ya ccm taifa.

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MKUTANO WA Empower Tanzania Inc.

Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na balozi wa Tanzania nchini Marekani bi. Mwanaidi Maajar jana katika mkutano wa Epower Tanzania Inc. Kulia ni mkurugenzi wa taasisi hiyo bi. Carlene Embreb hayo yote yalijiri jijini Des Moines Iowa.

MH. Kikwete ahudhuria mazishi ya mtoto wa Mwapachu

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh JK akiweka udongo kwenye kaburi la Harith J. Mwapachu ikiwa ni katika kushiriki kwake katika mazishi hayo. Harith Mwapachu alifariki mapema jana asubuhi jijini Dar es salaam na kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu hapo hapo jijini Dar es saalm.