Wednesday, 30 November 2011

DR. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAZIWA MAKUU - BURUNDI

 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr Kharib Bilal akihutubia mkutano wa Maziwa makuu uliofanyika Bujumbura Burundi jana.
 Makam wa rais wa tanzania Bilal (kushoto), makam wa rais wa Burundi bw. Therence (katikati) na mwenyekiti wa umoja wa Afrika (AU) bw. Jan Ping wakiwa wamesimama wakati wimbo maalum ukipigwa.
 Dr. Bilal alipokuwa akiwasili kwenye ukumbi tayari kufungua mkutano huo.
Waziri wa Afrika mashariki bw. Samwel Sitta kwa makini kabisa akimsikiliza makam wa rais Dr. Bilal.

JERRY MURO YU HURU TENA.

Ni baada ya mahakama ya Kisutu kukosa ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani.
Mtangazaji wa (TBC1) Jerry Muro akizungumza na wahandishi wa habari mara baada ya kuachiwa huru.
Murro na mkewe wakitoka mahakama ya kisutu.

Monday, 28 November 2011

TAARIFA MAALUM KWA VYOMBO VYA HABARI


Taarifa maalum iliyotolewa leo mara baada mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa Chadema na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete.

Mh. Kikwete, Mh Membe, Mh. Mbowe pamoja na profesa Mwesiga wakijadiliana jambo wakati wa mapumziko katika mkutano baina ya viongozi wa Chadema na rais Kikwete leo.

Monday, 14 November 2011

MH. MBUNGE M. DEWJI AKAGUA MRADI WA MAJI SINGIDA MJINI

Mbunge wa Singida mjini (CCM) Mh. Mohamed Dewji akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wanaoratibu na kusimamia mradi wa maji Singida mjini.
Mh. Mohamed Dewji al-maarufu kama 'MO' akikagua mradi huo unaofadhiriwa na BADEA.
Isaack Nyalonji ambae ni Mkurugenzi wa SUWASA akitoa maelekezo kwa Mbunge Mh. Dewji juu ya maendeleo ya mradi unaotarajiwa kukamilika mapema mwezi Julay mwakani

MVUA KUBWA YASABABISHA MAFURIKO MWANZA.

Ndege ya Precision air ikiwa kwenye maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza na kusabisha mafuriko katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa Mwanza.
Hivyo ndivyo uwanja wa ndege wa Mwanza ulivyoathirika kutoka na mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza.

MH. EDWARD LOWASA ACHANGISHA MIL 200

Mbunge wa Monduli na Waziri kuu mstaafu Mh. Edward Lowasa akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki pamoja wananchi kwa ujumla waliohudhuria haraambe kwa ajili kuchangisha fedha za ujenzi wa Kanisa katoliki ambalo linatarajiwa kuwa kubwa kuliko lolote katika ukanda wa ziwa Victoria na ujenzi huo utalighalimu kiasi shilingi milioni 700 . Harambe hiyo iliyoongozwa na Mh. lowasa ilifanikiwa kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 200 za kitanzania.
Mh. Edward Lowasa akinena jambo na Mjumbe wa Halmashauri kuu mkoa wa Mwanza Mh. Christopher Mwita.

Sunday, 13 November 2011

DR. SHEIN ZIARANI RAS AL KHAIMAH.

Rais wa Ras Al Khaimah Sheikh Said Bin Sagr Al Qasimi akiwa katika mazungumzo na Mgeni rais wa Zanzibar Dr. Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Shain akipewa maelezo juu ya utendaji na ufanisi wa Kampuni hiyo toka naibu mtendaji wa kampuni ya Ceramics Bw.Abdallah Massaada
Rais wa Zanzibar akitembeles vifaa kadha vinavyotengeza na Kampuni hiyo.

MH. JK AZINDUA MRADI WA UMEME AKIWA ZIARANI - IRINGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika kijiji cha Mawengi Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa leo
Mh. rais akipokea hotuba iliyosomwa kwake na bi. Alice Michellesi wa taasisi ya Acra iliyodhamini mradi huo wa umeme.
Kundi kubwa la wananchi wa kijiji cha Mawengi wakimshangilia Mh. rais alipokuwa akiwasili kijijini hapo leo,
Mh. JK Kikwete akiangalia ramani inayoonyesha michoro ya majengo na maelekezo mengine yanahusu mradi huo na eneo lake
Mh. rais akipata maelekezo ya namna mitambo hiyo inavyofanya kazi na uwezo wake kiutendaji ambao inakadiliwa kwamba itawahudumia wananchi wapata 10,000 wa vijiji vya Mawengi, Madunda na Lupande.
Katibu kiongozi Mh. Philemoni Luhanjo akiwasalimu wanakijiji wakati wa uzinduzi huo.
Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua mara baada ya kuwasili Mkoa Iringa ambako ulizinduliwa mradi wa Umeme.
Mh. rais Dr. JK Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watawa wa kanisa Katoliki la Mawengi baada ya uzinduzi wa mradi wa Umeme Kijijini hapo leo.

NAPE AZINDUA TAWI JIPYA LA CCM JIJINI DAR ES SALAAM


Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM-Taifa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama (NEC) Mh. Nape Nnauye akiwahutubia wanacha wa CCM walika katika uzinduzi wa tawi jipya la CCM katika mtaa wa Pamba House leo jijini Dar es salaam.

Katibu wa itikadi na uenezi ambae pia ni mjumbe wa ( NEC) Mh. Nape Nnauye akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa tawi hilo leo jijini Dar es salaam.

BALAMA NA MBILINYI WAMALIZA MGOGORO MBEYA.

 Mbuge wa Jimbo la Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akijiandaa kuwahutubia wananchi wa Mbeya mjini kufuatia vurugu zilizodumu kwa siku mbili ambazo zimesababisha kifo cha mtu mmoja ambae jina lake halijafahamika mpaka sasa.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mjini Bw. Evans Balama akimnong'oneza jambo Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Joseph Mbilinyi kabla mbunge huyo hajahutubia mkutano wa hadhari uliomaliza mgogoro uliopelekea vurugu zilizodumu kwa siku mbili Mjini humo. 

Friday, 11 November 2011

MWENYEKITI WA CCM - TAIFA DR. KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE WA CPC TOKA CHINA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Taifa Dr. JK Kikwete akizungumza na kiongozi wa msafara na ambae pia ni mjumbe wa NEC wa chama cha kikoministi cha China Liu Jiangxi.
Ujumbe wa chama cha Kikoministi cha China (CPC) ulipotembelea makao makuu ya zamania CCM Lumumba jijini Dar es salaam leo.
Katibu wa itikadi na uenezi CCM Taifa Nape NNauye kwa pamoja na ujumbe wa Chama Cha Kikominist cha China wakitoa heshima kwenye makaburi ya wataalam wa kichina Majohe, Gongo la Mboto jijini Dar es salaam leo.

TANZANIA NA CHINA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA UTALII

Bi. Maimuna Tarishi (mwenye miwani) ambaye ni katibu mkuu wa wizara ya Utalii akimkaribisha makamu wa gavana wa Jimbo la Jiangxi la China Wizarani hapo leo jijini Dar es salaam, na kulia ni afisa utalii wa wizara bi.Lilian Nyaki.
Makamu wa gavana wa Jimbo hilo Jiangxi akikabidhi kitabu chenye maelezo yanahusu vivutio vya utalii kwa mkurugenzi wa utalii bwana Ibrahim Mussa leo jijini dar es salaam.
Ujumbe kutoka Jimbo la Jiangxi China katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo yenye lengo la kutoa fursa kwa China kuwekeza katika sekta ya utalii.

MH. DR. KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO JIJINI DAR

Waziri machachari kabisa wa wizaraUshirikiano wa Afrika Mashariki na Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania Mh. Samweli Sitta akionyesha furaha yake alipokuwa akimkaribisha Dr. JK Kikwete kwenye mkutano wa kazi uliojulikana kama (Business Meeting) wenye lengo kujadili mpango wa uwekezaji katika kilimo.
Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukumbini Ubungo Plaza.
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Dr. JK Kikwete akihutubia ukumbini Ubungo Plaza leo Jijini Dar es salaam.
Wageni mbalimbali wakimsikiliza Dr. JK Kikwete alipokuwa akiwahutubia leo katika ukumbi wa Ubungo Plaza katika mkutano wa waliouita kuwa ni (Business Meeting) ambao umeandaliwa na TAFSIP
Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakimpigia makofi Dr. JK Kikwete alipokuwa akiwahutubia leo jijini Dar es salaam.

WAMACHINGA WALETA TAFLANI KATIKA SOKO LA MWANJELWA - MBEYA

Polisi wa kikosi cha FFU wakiwatawanya wafanayabiashara wa soko la Mwanjelwa walisababisha vurugu na upotevu wa amani katika eneo hilo leo mchana mjini Mbeya.
Hili ni kundi moja kati ya makundi kadhaa ya wafanyabiashara maarufu kama wamachinga wakijiandaa kuvaana na polisi baada ya jaribio lao la kutaka kuziharibu ofisi za watendaji wa Uyole na Sinde kwa madai kwamba ndio chanzo cha mateso wanayoyapata kutokana na uzembe wa viongozi wao kujikuta likizuiliwa na polisi wa kikosi cha FFU.
'Usalama kwanza' ndivyo wanavyoonekana kusema watu hawa ambao walilazimika kukimbia baada ya kukaidi agizo la polisi lililowataka kutawanyika na hivyo kuwaladhimisha polisi hao kutumia nguvu kuwatawanya. hapa ni wakati ambapo hali ikiwa tete kweli
Raia wakitawanyika kwa kasi ya ajabu kuokoa maisha yao kufuatia vurugu hizo leo.

Thursday, 10 November 2011

MJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA KIKOMINIST CHA CHINA AWASILI NCHINI TANZANIA

Katibu mkuu wa CCM Taifa Dr. Wilson Mkama akimlaki bwana Liu Yunshn ambae ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikominist cha China aliyewasili leo kwa ziara ya siku tatu.
Katibu mkuu wa CCM taifa Mh. Wilson Mkama akimtambulisha mjumbe wa Chama Cha kikominist Cha China (CPC) Liu Yunshan kwa Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mh. Nape mnauye alipowasili leo mchana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere. Kulia ni Katibu wa uchumi mipango na fedha wa CCM Bw. Mwigulu Nchemba.

MICHAEL NDEJEMBI APONGEZA UANZISHAJI WA TAWI LA CCM-NEW YOK

                   Mwenyekiti wa CCM Marekani bw. Michael Ndejembi

Mwenyekiti wa CCM  Marekani bwana Michael Ndejembi amepongeza hatua zilizofikiwa katika kuanzisha kwa  tawi la CCM New York. Akiongea na blog hii ya Chama leo asubuhi, bw. Ndejembi amesema hatua hiyo ni muhimu na kwamba inazidi kuiimarisha CCM kwa ujumla na itasaidia sana ustawi wa chama ndani na nje ya Tanzania.
Michael Ndejembi ambaye ndie mwanzirishi wa CCM hapa marekani ametaka pia miji mingine kuiga mfano wa wanachama hao wa New York katika kuanzisha matawi katika maeneo yao ili kusaidia mtandao huo CCM ambao ameuelezea kuwa umeanza kusambaa kwa kasi.

UJUMBE WA SONGAS WAMTEMBELEA MH. KIKWETE.

Mkurungenzi wa Songas Tanzania bw. Christopher Ford akikaribishwana rais JK ikulu jijini Dar es salaam leo.