Thursday, 10 November 2011

MICHAEL NDEJEMBI APONGEZA UANZISHAJI WA TAWI LA CCM-NEW YOK

                   Mwenyekiti wa CCM Marekani bw. Michael Ndejembi

Mwenyekiti wa CCM  Marekani bwana Michael Ndejembi amepongeza hatua zilizofikiwa katika kuanzisha kwa  tawi la CCM New York. Akiongea na blog hii ya Chama leo asubuhi, bw. Ndejembi amesema hatua hiyo ni muhimu na kwamba inazidi kuiimarisha CCM kwa ujumla na itasaidia sana ustawi wa chama ndani na nje ya Tanzania.
Michael Ndejembi ambaye ndie mwanzirishi wa CCM hapa marekani ametaka pia miji mingine kuiga mfano wa wanachama hao wa New York katika kuanzisha matawi katika maeneo yao ili kusaidia mtandao huo CCM ambao ameuelezea kuwa umeanza kusambaa kwa kasi.

No comments: